Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Sajid Ali Naqvi, Raisi wa Baraza la Maulamaa wa Kishia Pakistan, katika ujumbe wake kutokana na mnasaba wa kuingia mwezi wa Muharram al-Haram, amesisitiza kuwa kuandaliwa kwa vikao vya maombolezo ya Imam Hussein (as) ni haki halali, ya kisheria na ya kidini ya kila mwananchi, na kwamba ni wajibu kulinda heshima ya siku hizi tukufu, kuimarisha mshikamano wa Kiislamu, na kukabiliana na harakati zinazoleta fitina na kusambaratisha umoja.
Katika ujumbe huo, huku akiashiria wajibu wa pamoja wa maulamaa wa madhehebu mbalimbali, waimbaji wa nauha, na jamii kwa ujumla, amesema: Wote wanapaswa kwa kuheshimiana, kuchangia kuimarisha mazingira ya undugu, mshikamano wa Kiislamu na maisha ya pamoja yenye amani.
Mwanazuoni huyu mashuhuri wa Kipakistani ameeleza bayana kuwa: Mwezi wa Muharram si tu ukumbusho wa tukio lenye uchungu la Karbala, bali ni fursa ya kutafakari juu ya malengo, dira na ujumbe wa harakati ya Imam Hussein (as). Vikao vya maombolezo ni njia ya kuhuisha mwenendo wa Kihusseini na kufafanua sura halisi ya wapinga dhulma mbele ya watawala madhalimu wa kila zama.
Ni lazima kutumia fursa hii ya kiroho kwa kurejea masomo ya Ashura na kuchora njia za vitendo za kukabiliana na changamoto za zama zetu.
Maoni yako